Friday, October 28, 2011

UMUHIMU WA FASIHI

Fasihi ni mambo yanayotuwezesha sisi kama binadamu kuishi pamoja kwa uelewano. Kila jamii ulimwenguni ina njia zake muhimu zinazoiwezesha kupitisha fasihi kwa mila na desturi zao husika.

Kwa vitabu kadha wa kadha kuhusu fasihi, imegawanyika kwa sehemu mbili kuu.

a)Fasihi andishi
b)Fasihi simulizi.

Tukiangazia macho kidogo kwenye fasihi andishi twaoelewa ya kwamba hii hupitishwa kwa njia ya maandishi. Kwa mfano katika maabara kuna vitabu vingi vya hadithi fupifupi, tamthilia vitabu vya ngano na vingine vingi.

Vitabu hivi husaidia kupitisha mila kwenye binadamu. Vyaweza kuwa vya kuelimisha, kufurahisha, Kuonya au hata kupitisha ujumbe au hata kumpa mtu moyo wa kutenda jambo furani litakalowasaidia wengi katika jamii.

Kwenye aina ya pili, fasihi simulizi hupitishwa kwa njia ya maneno. Watu tofauti tofauti huweza kuelimisha jamii husika. Watu hawa kwa mfano: malenga hutunga shairi zinazopendeza na zitakazopitisha ujumbe tofauti.

Wengine hutunga nyimbo, ngano ambazo pia ni njia nzuri ya kupitisha ujumbe na kuelimisha jamii.

Mengi ya fasihi utaweza kuyapata kupitia kwangu katika uandishi utakaofuata hivi karibuni.

2 comments:

  1. ndio maana twapaswa kuwa tunaafikiana kila jambo linaloletwa kwetu kama jamii husika.

    ReplyDelete
  2. ungeeleza hii mada kwa ukamilifu

    ReplyDelete