Friday, October 28, 2011

JUSTICE MUST BE SEEN TO BE DONE

Jalia meona, mwajifanya wokovu,

Utu hamna, kwetu sisi ni hofu,

W’enda mchana, kutenda machafu,

Hela mwapata, kupita kiasi.



Adhuhuri mwaja , kupanga uongo,

Sisi twaomba, mtumie ubongo,

Wengi waumia, kwa kukosa jirongo,

Hela mwapata, kupita kiasi.



Mwaweka mjadala, ngwenje iongezwe,

Tayari, mesikia mola, mwajua wenyewe,

Zetu nyie mwapora, nani tumwangalie,

Hela mwapata, kupita kiasi.



Letu ni njaa, lenu ni shibe,

Mahindi yaja, m’sema itupwe,

Ninyi mwataka, wapi tuelekee,

Hela mwapata, kupita kiasi.



Twaomba Jalali, sisi atujalie,

Mwengine ni nani, ama tutulie,

Lakini mie najali, mfahamu nyie,

Hela mwapata, kupita kiasi.

No comments:

Post a Comment